momosgossip. Powered by Blogger.

Monday, July 23, 2012

MTOTO WA UWOYA NI WA DUDE ?


 Uwoya akiwa na Krish.
Eva akiwa na Naima.
Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Kulwa Kikumba 'Dude'.
Na Erick Evarist
AMA kweli duniani wawiliwawili na kama huna mwana eleka jiwe! Watoto wazuri wa mastaa wakubwa wa sinema za Kibongo, Irene Pancras Uwoya (Krish) na Kulwa Kikumba (Naima) wanafanana ileile, Ijumaa Wikienda limewakagua kuanzia nywele hadi kucha.
Awali ilikuwa vigumu kuwatathmini watoto hao kwa kuwa walikuwa wadogo lakini sasa wamekua hivyo wamependeza na ukibahatika kumuona mmoja halafu ukaletewa mwingine ni vigumu kuwatofautisha.
Baada ya kuwepo kwa habari za kufanana kwa watoto hao ambao wa Dude ana sura yenye mvuto ‘beautiful’ na wa Uwoya ‘handsome boy’, Ijumaa Wikienda lilizama kwenye makabrasha yake na kukagua picha moja baada ya nyingine ili kung’amua ukweli.
MAJIBU YA KUPERUZI
Katika kuperuzi na kuzidadisi picha za watoto hao, majibu yalionesha waziwazi kufanana kwao ambapo jamii inafahamu wazi ni wa uzao tofauti kabisa.
Uwoya alimzaa Krish na mumewe kipenzi ambaye ni msakata kabumbu wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ huku Dude akimzaa Naima na mkewe ‘Eva wa Dude’.
Viungo vingi vya miili yao vinafafa kiasi kwamba ukimuona wa Dude unaweza ukadhani ni wa Uwoya na ukimuona wa Uwoya ni ‘vaisivesa’. Wamefanana kuanzia nywele, midomo, mashavu, pua, macho, kucha, paji la uso na mikono yaani ni saresare maua.
NGOJA TUMTAFUTE DUDE
Baada ya kujiridhisha kufanana kwa Krish na Naima, paparazi wetu alimtafuta Dude (baba Naima) ambaye alikiri kuwepo marafiki zake wengi ambao wamekuwa wakimwambia na kumsifia kuwa mwanaye amefanana na Krish wa Uwoya.
“Kufanana ni kitu cha kawaida kabisa, mimi mwenyewe nimeshafananishwa sana na watu ambao wengine ukiambiwa unaweza kushangaa. Ni kweli mwanangu na wa Uwoya wanafanana.
“Wengi wamekuwa wakizungumzia sana kufanana kwa mashavu, midomo na viungo vingine, kitu ambacho mimi naamini kinaweza kutokea kwa mwanadamu yoyote,” alisema Dude.
RAFIKI WA DUDE
Staa mmoja mkubwa wa filamu ambaye ni rafiki wa Dude, alipofika kumtembelea hivi karibuni, nyumbani kwake Jeti Lumo jijini Dar, baada ya kumuona Naima na kwa kuwa anamfahamu Krish, alikiri kuwa kweli duniani wawiliwawili.
“Kusema kweli watoto hawa wa mastaa wamefanana kwa 150%, itapendeza sana kama siku moja nao watakuwa mastaa na ikiwezekana waje waoane kabisa,” alisema staa huyo.
MAMA KRISH YUPO WAPI?
Hata hivyo, jitihada za kumpata mama Krish ili kujua na yeye kama anaweza kutia neno lolote juu ya kufanana kwa watoto wao, hazikuzaa matunda, lakini akipatikana atawekwa hewani na mtazamo wake.
TUJIKUMBUSHE
Pamoja na kufanana kwa kupita maelezo, watoto hao wametofautiana siku ya kuzaliwa kwani Krish wa Uwoya alizaliwa Mei 8, 2011 huku Naima wa Dude akizaliwa Machi 14, mwaka huu.
KALAMU YA MHARIRI

0 comments:

Post a Comment