momosgossip. Powered by Blogger.

Saturday, October 27, 2012

MAIMATHA ATIMULIWA KWENYE KIBAO KATA YA AUNT EZEKIEL




MTANGAZAJI wa Kipindi cha Ben & Mai kinachorushwa hewani na TBC1, Maimartha Jesse hivi karibuni alipata aibu ya mwaka baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya Ukumbi wa Budha Blue, Mikocheni, Dar kwenye sherehe ya ‘kibao kata’ cha nyota wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel.


Habari zinadai kwamba Mai alikutwa na ishu hiyo kwa sababu hakuwa ametoa mchango uliokuwa umepangwa kwa ajili ya kuingia kwenye sherehe hiyo.


Mai akiwa amevalia sare ya sherehe hiyo, alikataliwa getini na mlinzi ambaye alimtaka aoneshe kadi au ujumbe wa simu ‘SMS’ aliotumiwa kwenye simu yake wa kumwalika ambapo vyote hakuwa navyo hivyo kutimuliwa
 
HIZI NDIZO PICHA ZA KIBAO KATA







Picha ni kwa hisani ya GUMZO LA JIJI BLOG

0 comments:

Post a Comment